Mke wa Rais wa Nigeria, Hajiya Aisha Buhari, Baraza la mawaziri pamoja na wanachama 3000 watakutana katika mkutano wa wanawake utakaofanyika nchini Nigeria ukiwa na lengo la kuhamasisha na kudumisha amani ikiwa ni pamoja na kutatua migogoro nchini humo.
Mkutano huo utafanyika siku ya Jumatatu ya Tarehe 19 machi mwaka huu huko Nigeria Abuja.
Mrs Onyechere ambaye ni katibu Mtendandaji wa kituo cha jinsia ameweka swala hilo wazi na kusema kuwa, mkutano huo utafanyika siku nne kuanzia Machi 19 hadi machi 22 katika ukumbi wa Shehu Musa Yar’Adua.
Amesema kuwa Mkutano huo utaenda na sera ya Amani Nigeria.
Aidha mkutano huo umeandaliwa na kituo cha mambo ya jinsia cha kimataifa kwa kushirikiana na kampuni ya National Orientation Agency (NOA) inayojihusisha na uhamasishaji wa sera za nchi, Uzalendo, kujenga umoja na Maendeleo ya jamii ya watu wa Nigeria.
Kumekuwa na matukio ya kikatili yanayoendelea nchini humo yakionesha mvurugiko wa amani ya nchi hiyo, hivyo wanawake hao wakiongozwa na mke wa Rais wameamua kufanya mkutano huo wa kuhamasisha amani.