Mke wa mhubiri maarufu wa Nigeria, T.B Joshua, Bi. Evelyn Joshua ameeleza namna amefanya mahojiano maalum na gazeti la Sun na kueleza namna alivyoanza uhusiano wa mapenzi na mumewe pamoja na maisha yao ya mapenzi kama wana ndoa.

Evelyn alieleza kuwa alipokutana na T.B Joshua kwa mara ya kwanza alimwambia bila kumung’unya maneno kuwa anataka kumuoa (ali-propose).

Haya ni baadhi ya maswali na majibu ya mahojiano hayo: 

Sun: Tuambie mlikutanaje

Evelyn: Ndio.. kama nilivyokwambia mwanzo ndivyo ilivyo. Mhhh, sijui niiteje… ulikuwa mpango wa Mungu. Ni hadithi ndefu lakini kitu cha kushangaza zaidi siku hiyo kilikuwa hicho. Ilikuwa siku niliyokutana naye na ndio siku aliponiomba tuoane. Alisema nakupenda, nataka kukuoa. Ilikuwa kama hivyo tu.

Sun: Watu wengi wanaamini kwamba wachungaji sio ‘romantic’. Wanafunga na kuomba muda wote. Je, T.B Joshua ni ‘romantic’?

Evelyn: Ni mwanaume mzuri

Sun: Ni mwanaume mzuri kitandani?

Evelyn: Mhhhhh..! Siwezi kusema, nisingejua… kwa sababu hakuna mwanamke ambaye angependa kumzungumzia mumewe hadi kwenye hatua hiyo. Ila mimi nadhani ni mwanaume mzuri.

Sun: Watu wengi hawamuelewi mumeo, wanadhani ni mtu mwenye mambo ya nguvu za giza na anatumia nguvu za giza. Unaposoma habari kama hizo unajisikiaje?

Evelyn: Najua sio kweli, hawamjui. Sio mtu wa ajabu, sio mtu wa nguvu za giza, amejitoa kwa kazi yake tu. Ni mtu ambaye ana hofu ya Mungu ndani yake, ni hivyo tu. Hizo habari hazinitingishi kwa vyovyote kwa sababu inaonekana hawamfahamu.

-Evelyn ambaye ana watoto watatu wa kike pekee, ameeleza kuwa ameridhika na ndoa yake na wanae wa kike wa pekee kwa kuwa amezungukwa na wavulana. Alieleza kuwa haoni kuwa na watoto wa kike pekee kama tatizo ingawa jamii yake huthamini watoto wa kiume zaidi ya watoto wa kike.

Nape Atolea Majibu Taarifa Ya kupiga Marufuku Vimini, Mlegezo
Filamu Mpya ya Star Wars aliyoigiza Lupita Nyong'o yavunja Rekodi Za Mauzo, Angalia Trailer Hapa