Mke wa Beki wa Chelsea Thiago Silva amekanusha taarifa za mwenziwake kuwa mbioni kuihama klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu.
Belle Silva amekanusha taarifa hizo, baada ya kusambaa kwa kasi kubwa tangu mwishoni mwa juma lililopita.
Beki huyo mwenye umri wa miaka 38, amekuwa na mchango mkubwa tangu alipojiunga Chelsea mwaka 2020 na akaweka rekodi ya kucheza jumla ya mechi 115.
Silva aliisaidia Chelsea kubeba ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu wa 2020-2021 na kupewa unahodha wa timu wakati Cesar Azpilicueta akiwa nje ya uwanja.
Vile vile, Silva amekuwa akianzishwa katika kikosi cha kwanza mara kwa mara tangu alipotua The Blues.
Beki huyo alipewa sifa baada ya kuonyesha kiwango bora kwenye michezo ya Ligi Kuu ya England tangu alipojiunga Chelsea mwaka 2020 na akaweka rekodi ya kucheza jumla ya mechi 115.
Belle Silva aliandika katika ukurasa wake wa Instagram baada ya mchezo wa mwishoni mwa juma lililopita dhidi ya Nottingham Forest iliyoilazimika Chelsea sare ya 2-2.
“Ningependa kusema asante kwa upendo mkubwa, mmetuonyesha heshima kubwa, najua msimu bado haujaisha, msimu ulikuwa mbaya kwetu, tunaipenda Chelsea na tutaisapoti miaka yote,” aliandika mke wa Silva.
Silva ataiongoza Chelsea katika mechi zao zilizobaki za ligi dhidi ya Manchester United, Manchester City, kabla ya kumenyana na Newcastle.