Melania Trump, mke wa Rais wa Marekani, Donald Trump amesema kuwa yeye ni mtu aliyenyanyaswa zaidi duniani kupitia mitandao ya kijamii.

Kauli hiyo imesikika katika kipande cha mahojiano aliyofanya na shirika la habari la ABC News, yaliyofanyika hivi karibuni wakati wa ziara yake barani Afrika.

“Mimi naweza kusema ni mtu niliyenyanyaswa zaidi kwenye mitandao. Mimi ni mmoja kati yao [waliowahi kunyanyaswa zaidi] kama utaangalia kilichosemwa kuhusu mimi mitandaoni,” alisema.

Alifafanua kuwa hiyo ndiyo sababu iliyomfanya aanzishe kampeni ya ‘Be Best’ ambayo inajikita zaidi katika kuelimisha kuhusu masuala ya mitandao na tabia zake.

ABC walitoa kionjo kifupi cha mahojiano na Mke wa Rais Trump na wamepanga kuachia video ya mahojiano yote leo.

Melania anazuru nchi za Afrika ikiwa ni pamoja na Misri, Ghana, Malawi na Kenya. Mashambulizi na ukosoaji unaomuandama kwenye mitandao ya kijamii dhidi yake vinaweza kuwa sababu ya kujiweka katika nafasi hiyo kutokana na majeraha ya kisaikolojia yatokanayo na mashambulizi hayo.

Video: Msaidizi wa Mwalimu afichua siri, Maswali yenye utata kutekwa kwa Mo Dewji
Jarida lililoibua tuhuma za ubakaji dhidi ya Ronaldo lawa 'ngangari'