Mke Mlinda Lango wa zamani, Edwin van der Sar, Annemarie amefichua hali ya maendeleo ya kiafya ya mumewe tangu alipokumbwa na tatizo la damu kuvuja kwenye ubongo.
Van der Sar mwenye umri wa miaka 52, alikumbwa na tatizo hilo wakati alipokuwa mapumzikoni huko Croatia, juma lililopita. Van der Sar alikimbizwa hospitali na tangu siku hiyo alilazwa kwenye wodi ya wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu.
Kwa maclezo yake yaliwekwa bayana kupitia ukurasa wa mitandao ya kijamii wa klabu ya Ajax, mrembo Annemarie alisemwa mumnewe ameanza kuwasiliana, aliposema: “Edwin bado yupo kwenye wodi ya wasotencemaa. Maisha yake maalumnu, lakini hali yake hayapo kwenye hali ya hatari. Mara zote tunazokwenda kumwona, anawasiliana. Tunasubiri kuona jinsi hali hiyo inavyoendelea.”
Kipa huyo Mdachi aliwahi kuzichezea Ajax, Juventus, Fulham na Manchester United na kipindi cha karibuní alikuwa akifanya kazí kama mkurugenzi kwenye klabu ya Ajax kabla ya kung’atuka mwaka huu.
Kwa wakati wake aliokuwa Old Trafford, Van der Sar aliisaidia Man Uníted iliyokuwa chini ya kocha Sir Alex Ferguson kushinda matají manne ya Ligi Kuu England na Ligi ya Mabino Ulaya mara moja 1 2008.
Alicheza mechi 266 kwenye kikosí cha Man United kabla ya kustaafu mwaka 2011 na nafasi yake kurithiwa na kipa David de Gea, ambaye kwenye dirisha hili la majira ya kiangazi amefunguliwa mlanggo wa kutokea baada ya mkataba wake kufika tamati huko Old Trafford.
Van der Sar na mrembo Annemarie wapo kwenye ndoa kwa miaka 17. Kwenye uhusiano wao wamebahatika kupata mtoto wa kiume, Joe, 25, ambaye ní kipa wa Pittsburgh Panthers.