Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Dkt. Pindi Chana amemteua Brigedia Jenerali, Mbaraka Naziad Mkeremy kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS),
Balozi Chana amefanya uteuzi huo hii leo Septemba 23, 2022 kwa mamlaka aliyopewa chini ya Kifungu cha 5(1) na 5(4) cha Sheria ya Wakala za Serikali Sura ya 245, ambapo pia amewateua wajumbe wanne wa bodi ya Wakala wa Huduma za Misitu nchini.
Amewataja wajumbe hao kuwa ni Mkurugenzi wa Utafiti na Uzalishaji wa Misitu, Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI), Dkt. Siima Salome Bakengesa, na Mkurugenzi Msaidizi – Uchumi na Uzalishaji, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Eng. Enock Nyanda Emmanuel.
Wengine ni Mkurugenzi wa Uhusiano, Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Adv. Piensia Christopher Kiure na Afisa Mwandamizi, Ofisi ya Rais, CPA. Bahati Lucas Masila.
Kwa mujibu wa Kifungu cha 5(5) cha Sheria ya Wakala za Serikali Sura 245, Prof. Dos Santos Aristariki Silayo, Kamishna wa Uhifadhi – TFS, anakuwa Katibu wa Bodi hiyo na uteuzi huo ni wa miaka mitatu ukianza rasmi hii leo Septemba 23, 2022 hadi eptemba 22, 2025.