Mkoa wa Pwani unakabiliwa na uhaba wa vyumba vya madarasa 3,973 hali ambayo inasababisha wanafunzi zaidi 200 kwenye darasa moja.

Hayo yamesemwa na Afisa Elimu mkoa wa Pwani, Germana Sendoka wakati akitoa hali ya kitaaluma na changamoto wanazokabiliana nazo.

Amesema kuwa mkoa huo una jumla ya vyumba vya madarasa 3,003 huku mahitaji ya vyumba yakiwa ni 6,976 ili kuweza kukidhi mahitaji, pia upungufu wa nyumba za waalimu ni 4,811 huku zilizopo ni 1,798 pekee.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo amesema pamoja na juhudi zinazofanywa na Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuongeza miundombinu ya shule lakini bado miundombinu hairidhishi.

 

Infantino afanya mabadiliko makubwa ndani ya FIFA
Vijana watakiwa kujifunza historia ya nchi na viongozi wao