Uongozi wa klabu ya Newcastle United umekubali kumsajili beki kutoka Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo, Chancel Mbemba Mangulu akitokea klabu ya Anderlecht ya nchini Ubelgiji.

Newcastle Utd waliafiki makubaliano na viongozi wa klabu ya Anderlecht mwishoni mwa juma lililopita na kwa sasa kinachohangaikiwa huko St James Park ni kibali cha kufanyia kazi cha beki huyo mwenye umri wa miaka 20.

Tayari mkongoman huyo ameshakubalian na viongozi wa klabu Newcastle Utd maslahi binafsi na kama mipango ya utafutwaji wa kibali chake cha kufanyia kazi itakwenda vyema huenda akaanza kuonekana kikosini mwishoni mwa juma lijalo ambalo ligi ya England itakua ikianza rasmi.

Mbemba anakuwa mchezaji wa tatu kusajiliwa na The Magpies chini ya utawala mpya wa meneja kutoka nchini England, Steve McLaren baada ya kusajiliwa kwa kiungo nchini Uholanzi Georginio Wijnaldum pamoja na mshambuliaji kutoka nchini Serbia, Aleksandar Mitrovic.

Mbemba anaondoka nchini Ubelgiji akiacha kumbukumbu ya kuitumikia Anderlecht katika michezo 28.

Ukawa Wamvua Lowassa Taji La Miba
Martinez Atamba Kuiletea Kombe Atletico Madrid