Kiungo wa Arsenal mjerumani Mesut Ozil ameibuka na kuamua kuvunja ukimya juu ya yale yanayoitokea klabu ya Arsenal. Ozil amekuwa akilaumiwa na wachezaji wakongwe wa klabu hiyo kwa kucheza chini ya kiwango lakini amewaambia wachezaji wakubwa wa klabu hiyo kwamba waache maneno waiunge mkono timu.

Mchezaji huyo hakutaja jina moja kwa moja la mchezaji wa zamani wa Arsenal lakini ni wazi kwamba ujumbe huo uliwaendea Martin Keown, Ian Wright na Thiery Henry ambao mara nyingi ndio wamekuwa wakizungumza sana kuhusu Arsenal.

Ian Wright ameupata ujumbe wa Ozil na ameamua kumjibu kwa kumuambia kwamba aache kujificha katika kivuli cha Alexis Sanchez badala yake kama kweli anaipenda sana klabu ya Arsenal kama anavyodai basi ashike kalamu asaini mkataba mpya.

“Kama una mapenzi mema na klabu kwanini hujasaini mkataba mpya? Ozil anajificha tu katika kivuli cha Alexis Sanchez kwa kuwa yeye ndiye mkataba wake unaongelewa sana lakini bado hajasaini mkataba mpya” alisema Wright.

Wright aliongeza kuwa wachezaji wa klabu hiyo hawajitumi kwa ajili ya kocha wao na ndio maana ahata akishambuliwa kimaneno wenyewe huwa hawajisikii vibaya wanacheza tu watakavyo.

Mchezaji huyo wa zamani wa Arsenal ambaye kwa sasa ni mtangazaji wa redio amesisitiza kwamba wao kama wachezaji wa zamani wa klabu hiyo wana uchungu mkubwa na Arsenal na ndio maana wanaongea mabaya yao ili kuwafanya wajirekebishe na kuwa bora.

Acacia kupunguza wafanyakazi migodini
Riyad Mahrez aliponzwa na tamaa za kwenda Old Trafford