Kiungo wa Simba, Jonas Mkude amekanusha taarifa zinazoenea mitandaoni kuwa hatacheza tena timu ya Taifa

Mkude ameeleza kuwa amepanga kukutana na kocha mkuu wa Taifa Stars, Etienne Ndayiragije, ili kumueleza tatizo lililomfanya ashindwe kuripoti kambini

Kuhusu suala lililoelezwa na Juma Ndambile, Mkude amesema wakala wake ni Paul Metchell, Raia wa Uingereza, hivyo hakuna ukweli wowote katika maelezo yaliotolewa na Ndambile.

Gazeti la Mwanaspoti leo limeripoti kuwa Juma Ndambile ambaye ni Meneja wa Kiungo wa klabu ya Simba Jonas Mkude amesema kuwa mteja wake JONAS MKUDE  hataichezea tena timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) akidai kuwa hafurahishwi na baadhi ya mambo ndani ya timu hiyo, ambayo atayaweka wazi akitakiwa kufanya hivyo.

Mwana FA athibitisha kuwa na virusi vya Corona
Manara: Nipo salama, nitapima Corona nikirudi Bongo

Comments

comments