Mkurugenzi wa Shirika la Ndege nchini (ATCL), Mhandisi Ladislaus Matindi amekanusha taarifa kuwa, ndege ya Dreamliner 787-8 ina hitilafu na kwamba ilisitisha safari yake ya Mwanza – Dar kuanzia juzi.
Amesema katika ndege nne za ATCL (3-Bombardia na 1-Dreamliner), Bombardia zinaendelea na safari bila matatizo ila Dreamliner imesimamishwa kwa makusudi ili ifanyiwe matengenezo kwani kwa sasa ipo katika majaribio
Marekebisho hayo ni kama ya WIFI na mengine madogo madogo yanayohusu uendeshaji wa ndege maana safari za ndege hiyo kwa sasa ni za majaribio kwa ndege yenyewe na Marubani pia.
Aidha, amesema kuwa walipanga marekebisho hayo kufanyika wiki tatu baada ya kuanza safari zake, ila kilichopelekea marekebisho ya ghafla ni mafundi waliomba yafanyike mapema kwa kuwa wanaondoka nchini.
-
Maafisa Madini wapewa somo utoaji wa leseni
-
Video: Lissu narudi nyumbani, CCM waandamana kumpinga mbunge aliyeitosa Chadema
-
DC Joketi: Sheria itachukua mkondo wake kwa atakaye kaidi agizo
Hata hivyo, marekebisho hayo yaliyoanza juzi yanatarajiwa kukamilika leo na hivyo ndege hiyo kuanza safari zake kama kawaida hapo kesho.