Mkurugenzi Mkuu wa Acacia nchini Tanzania, Brad Gordon na Mkurugenzi Mkuu wa fedha, Andrew Wray, wamejiuzulu nyadhifa zao ingawa bado watakuwa chini ya kampuni mpaka mwisho wa mwaka huu,.

Taarifa ya kujiuzulu kwa viongozi hao imetolewa leo na kampuni hiyo na kusema kuwa Mkurugenzi Mkuu, Brad Gordon anarejea nyumbani kwake Australia na Andrew Wray anatafuta fursa mahali kwengine.

Aidha, tayari Bodi ya Acacia imewataja watu ambao watachukua nyadhifa za wawili hao, ambao ni Peter Geleta ambaye atakuwa Mkurugenzi Mkuu na Jaco Maritz atakachukua nafasi ya Andrew Wray aliyekuwa Mkurugenzi wa fedha.

Peter ambaye ametajwa kuwa na uzoefu kwenye uchimbaji madini kwa muda wa miaka 35 ameshawahi kufanya kazi na mgodi wa Anglo Gold Ashanti kwa miaka 25 na kampuni ya Barrick, na alijiunga na Acacia mwaka 2012 na alishawahi kuwa Meneja Mkuu kwenye mgodi wa Bulyanhulu.

 

James Collins aibwaga Wales, Chris Coleman asikitika
Benedictor Tinocco awajibu wanaoibeza Mtibwa Sugar