Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Rombo na watendaji wake wamejikuta matatani mara baada ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Selemani Jafo kuonyesha kukerwa na kutoridhishwa na kasi ya utendaji kazi wao.
Hali hiyo imejitokeza leo wakati alipokuwa katika ziara yake ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo iliyopo mkoani Kilimanjaro.
Amesema Halmashauri ya wilaya ya Rombo ni miongoni mwa Halmashauri zilizopokea fedha za awamu ya kwanza ya uboreshaji vituo vya afya lakini licha ya kupokea fedha hizo bado wapo nyuma ukilinganisha na halmashauri zingine zilizopata fedha kwa wakati mmoja.
Aidha, Jafo amemtaka mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kufanya kazi kwa weledi na kuwapa ushirikiano wa kutosha watendaji walio chini yake ili waweze kumaliza kazi hiyo kabla Februari 25, mwaka huu.
-
Ziara ya Majaliwa yang’oa kigogo Mara
-
Jaji Mkuu atoa angalizo kwa viongozi na wanasiasa
-
Serikali kuendesha mnada wa meno ya Viboko
Hata hivyo, amewapongeza Mkuu wa wilaya ya Rombo, Agness Hokololo na Katibu Tawala wake wa wilaya, Asenga kwa kazi kubwa wanayofanya ya kusimamia maendeleo ya wilaya hiyo.