Aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dkt. Hussein L. Kidanto ameandika historia katika uongozi wa Rais John Magufuli baada ya kuwa mtumishi wa kwanza wa umma kuwajibishwa na Rais huyo kutokana na utendaji mbovu.

Rais Magufuli alimuondoa Dkt. Kidanto katika nafasi ya Ukaimu Mkurugenzi aliyokuwa na kumhamishia katika Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ambako atapangiwa kazi nyingine, baada ya kutoridhishwa na utoaji huduma katika hospitali hiyo ikiwa ni pamoja na kutofanya kazi kwa mashine za CT-Scan na MRI kwa kipindi cha miezi miwili bila sababu za msingi huku mashine za hospitali binafsi zikifanya kazi.

Rais aliyabaini hayo baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika hospitali hiyo. Kufuatia hatua hiyo, alimteua Profesa Lawrence Mseru kuwa Kaimu Mkurugenzi wa hospitali hiyo na kuivunja Bodi ya Wakurugenzi ya hospitali hiyo ambayo ilikuwa imemaliza muda wake.

Baada ya hatua hizo, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue alitangaza kuwa kila hospitali ihakikishe kuwa inatenga bajeti ya kufanyia ukarabati vifaa vyake ili kuepuka kuwakosesha huduma za msingi wananchi kwa sababu za kuharibika kwa mashine hizo.

Ronaldo Azindua Filamu Yake Jijini London
Yametimia, David Moyes Hana Kazi Hispania