Katika hali ya kushangaza, mikutano ya Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo – CHADEMA, Tundu Lissu inadaiwa kuzidi kukosa mvuto kutokana na wafuasi, wanachama na Watanzania kwa ujumla kujitokeza kwa idadi ndogo wakati kiongozi huyo akifanya mikutano yake.
Lissu yupo kwenye ziara zake za Kanda ya Ziwa kukutana na wanachama pamoja na Watanzania kama njia ya kuijenga CHADEMA sanjari na kuzungumzia mwelekeo wa Mkataba wa Bandari dhidi ya Dubai Ports World (DPW).
Katika mkutano uliofanyika hii leo Wilayani Bukombe Mkoani Geita, Lissu anadaiwa kushindwa kuvutia watu wa kwenda kumsikiliza, jambo linaloonesha mwelekeo mbaya wa chama hicho katika ujenzi wa hoja zenye ushawishi.
Inadaiwa kuwa, hoja ya DP World inayowatesa CHADEMA kwa sasa ni namna ya kuwaaminisha Watanzania kuhusu mchakato wa uwekezaji wa Bandari, huku wakitumia muda mwingi kuwasema Viongozi wa Serikali na wastaafu, hali inayodaiwa kuwapa wakati mgumu kuvutia watu kwenye mikutano yao.