Mkuu wa Shule ya Polisi Tanzania (Commandant TPS- Moshi), SACP. Ramadhani Mungi amewakumbusha na kuwataka wachezaji wa Timu ya Polisi Tanzania kuweka Juhudi zaidi katika Michezo yao, ili kuiwezesha timu hiyo kurejea na kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya Tanzania msimu ujao.

SACP Mungi ameyasema hayo hii leo Agosti 9, 2023 katika Ukumbi wa Mikutano uliopo Shule ya Polisi Tanzania, na amewakumbusha kuwa Jeshi hilo lina imani na timu hiyo, huku akiwataka wachezaji hao kuweka juhudi na jitihada, ili kukamilisha ndoto ya kutwaa ubingwa wa ligi hiyo pindi watakapo rejea.

Amesema, yeye aliwahi kucheza mpira wa Miguu mwaka 1998 na alicheza kwa mafanikio makubwa ambapo amewataka kuonyesha kiwango kwa daraja hilo walilopo sasa baada ya kushuka kutoka ligi Kuu.

Aidha, Mungi pia amewakumbusha kuwa mpira ni kazi ambayo inataka nidhamu na kuonyesha ushirikino (team work), ili kufikia malengo ambayo mashabiki na Timu hiyo wanatani kuyaona huku Mkuu huyo wa Shule ya Polisi Tanzania akiahidi kutoa ushirikiano,pamoja na maafisa kutoka Shule hiyo.

Amsha Mzuka Sh. Milioni moja na Smartphone toka Parimatch
Mazingira Hospitali ya Dodoma yawavuta Wanandoa