Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron kupitia ukurasa wake wa Twitter ameandika kuwa mkuu wa kundi la Dola la Kiislamu tawi la eneo la Sahara Afrika Magharibi ISGS, Adnan Abu Walid-Sahrawi ameuwawa na wanajeshi wa Ufaransa.
Aidha Macron amesema, kuuwawa kwa mkuu huyo wa kundi hilo la kigaidi ni mafanikio mengine makubwa katika mapambano dhidi ya makundi ya kigaidi katika eneo la Sahel.
Hata hivyo Kundi hilo linalaumiwa kwa mashambulizi mengi ya kigaidi yanayofanywa nchini Mali, Niger na Burkina Faso.
Kundi hilo liliwalenga wanajeshi wa Marekani katika mashambulizi ya mwaka 2017. Agosti mwaka 2017 nchini Niger, huku mkuu wa kundi hilo la kigaidi aliagiza kuuwawa kwa wafanyakazi 6 wa mashirika ya kutoa misaada kutoka Ufaransa, pamoja na madereva wao na waliokuwa wasaidizi wao raia wa Niger.