Mkuu wa Majeshi na Kiongozi wa Sudan, Jenerali Abdel Fattah al-Burhan ametahadharisha kwamba huenda vita vya nchini mwake vikaweza kuenea kwenye eneo lote la nchi zinazopakana na Sudan.
Akilihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Jenerali Burhan, amesema vita hivyo kati ya pande mbili hasimu za jeshi ni kama cheche inayoweza kuwasha moto kwenye ukanda wa nchi zinazopakana na Sudan.
Wakati huo huo, Jenerali Burhan ameitaka pia Jumuiya ya Kimataifa, ikijumlishe Kikosi cha Msaada wa Haraka – RSF, kwenye orodha ya makundi ya kigaidi na kuwakabili wanaofadhili kikosi hicho walioko nje ya mipaka ya Sudan.
Agosti 28, 2023, Umoja wa Mataifa ulitahadharisha kwamba vita na njaa vinatishia kuiteketeza Suda. Wakati huo mtawala wa kijeshi wa Sudan Jenerali Abdel Fattah al-Burhan ametembelea kambi za jeshi nje ya mji mkuu, Khartoum.