Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge, amefanya ziara katika masoko na mitaa ya Manispaa ya Singida ili kubaini hali halisi ya maeneo hayo na changamoto zinazowakabili wafanyabiashara wadogo maarufu kama wamachinga.

Ziara hiyo iliyoshirikisha Kamati ya Usalama ya Mkoa na viongozi mbalimbali wa Manispaa hiyo ililenga kubaini maeneo yenye changamoto kwa wafanyabiashara wenye maduka na wanaopanga bidhaa barabarani.

Akiwa katika ziara hiyo RC Mahenge amewataka Wakurungezi na wakuu wa Wilaya kuhakikisha zoezi la kuwahamisha wafanyabiashara hao linafanyika kwa njia yamajadiliano badala ya kutumia nguvu.

Mahenge amesema mchakato wa kubaini maeneo mapya ya kufanyia biashara na mipango ya kufunga baadhi ya barabara kwa nyakati tofauti inafanyika ili kuhakikisha kila mfanyabiashara anaendelea na shughuli zake bila kubuguziwa.

Watu 19 wakamatwa kwa tuhuma za uwizi
Sudan yazima mapinduzi yakijeshi