Kasi ya uchapakazi wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda iliyovuta usikivu wa Rais John Magufuli umesababisha Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigela kujipima kupitia yeye.

Shigela amesema kuwa kazi anayofanya Makonda katika mkoa wa Dar es Salaam kwa kuwashirikisha wananchi katika maendeleo ya sekta ya elimu ni sawa na ile anayoifanya katika mkoa wake.

Amesema tofauti ya kasi hiyo ni uwezo wa wananchi kifedha katika mkoa husika huku akikumbushia jinsi ambavyo Rais Magufuli alivyomsifu mkuu wa Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga kwa kufanikisha ujenzi wa madarasa kwa kuwashirikisha wananchi.

“Inategemea hali ya watu katika eneo husika. Kama wapo wananchi katika mkoa wako ambao mtu mmoja anaweza kuchangia shilingi milioni 10 kama kwa RC makonda ni vyema,” Shigela anakaririwa na Mwananchi.

“Lakini kama wananchi uwezo wao ni kuchangia tofali tano tunawatumia hao hao, na hapa Tanga tumefanikiwa kwa kiasi kikubwa,” aliongeza.

Akifungua mkutano mkuu wa ALAT jana jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli aliwataka wakuu wa mikoa mingine kuiga mfano wa Makonda kwa kuwashirikisha wananchi katika shughuli za kukuza sekta ya elimu nchini.

Mfalme ahimiza viboko mashuleni!
Lukaku akana mashtaka yanayomkabili