Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira amevunja bodi ya Benki ya Ushirika (KCBL) uamuzi uliokwenda sambamba na maazimio ya mkutano mkuu wa wanahisa uliofanyika Septemba 11, 2018.

Mghwira alitangaza uamuzi huo jana Desemba Mosi, 2018 na kutangaza kamati ya mpito itakayosimamia benki hiyo kwa kipindi cha miezi mitatu tangu alipotangaza.

“Nimeamua kuivunja bodi ya Benki ya Ushirika kutokana na maamuzi ya mkutano mkuu wa wanahisa ulioamua kuihamisha benki hii kutoka mfumo wa ushirika na kuirejesha katika mfumo wa kawaida wa uendeshaji wa mabenki chini ya utaratibu wa Benki Kuu,” amesema Anna Mghwira.

Aidha, amebainisha kuwa uamuzi huo umeitoa benki hiyo katika mfumo wa ushirika na hivyo ofisi ya mrajisi wa vyama vya ushirika imekosa uhalali wa kuisimamia.

Hata hivyo, ameongeza kuwa wakati wote wa zoezi hilo ofisi ya mrajisi pamoja na watumishi wake hawajaonyesha dhamira ya dhati ya kuifufua benki ama kuiongezea mtaji.

‘Marufuku daladala kuingia katikati ya jiji, watu wafanye mazoezi’
Suala la ushoga kwa 'Makasisi' lampa wasiwasi Papa Francis