Mkuu wa Shule ya Sekondari Masaki Wilayani Kisarawe, Hillary Bwagidy anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kubaka wanafunzi wa kike wa kidato cha Nne waliopo kwenye Kambi ya masomo shuleni hapo.
Mkuu wa Shule hiyo amekuwa akilalamikiwa na wanafunzi wa kike waliopo kwenye Kambi ya masomo kwamba amekuwa akiwaita mmoja mmoja nyumbani kwake nyakati za usiku na kuwalazimisha kuingia chumbani na kuwavua nguo Kwa lazima na kutimiza haja Zake , wanafunzi kadhaa tayari amefanikiwa kuwabaka kuwatolea vitisho vikali.
Mapema wiki iliyopita Mkuu wa Shule hiyo alimuita mwanafunzi mwenye imani ya kiislamu nyumbani kwake, akamwamuru Aingie sebuleni, baadae akamwamuru aingie chumbani na avue nguo zote amtengenezee dawa kwakuwa amekuwa akipatwa na homa mara Kwa mara, msichana huyo aligoma kutekekeleza matakwa ya mwalimu huyo alilazimisha bila mafanikio na kumwamuru atoke ila asithubutu kusema.
Mwanafunzi huyo hakuvumilia yaliyomkuta akaenda kuwasimulia wenzake. Wanafunzi wote wa kidato cha nne wakaanzisha mgomo wa kuingia darasani hadi hapo Afisa Elimu wa Wilaya ya kisarawe alipoitwa kusuluhisha mgogoro huo.
Juhudi za Afisa Elimu wilaya haikusaidia Kitu, Headmaster huyo aliendelea kuwatishia wanafunzi na kuwapa adhabu Kali.
Leo jumatatu Aprily 30 , 2018 wanafunzi wote wa kidato cha nne wameandamana kwenda ofisi ya kata wakitaka kuonana na Mkuu wa Wilaya ya kisarawe kueleza kero wanazopata toka Kwa mkuu wao wa shule na wako tayari kufika kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli.