Straika nyota nchini Mbwana Samatta anayekipiga katika kikosi cha TP Mazembe, ameteuliwa kuwa nahodha moywa wa kikosi cha Taifa Stars.
Uteuzi huo unahitimisha zaidi ya miaka mitano ya unahodha wa Stars kwa Nadir Haroub ‘Cannavaro’ ambaye ni nahodha wa Yanga pia Zanzibar Heroes.
Kocha wa Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa, amesema Samatta ndiye nahodha mpya wa kikosi chake.
“Samatta ndiye nahodha mpya wa Taifa Stars, haya ni mabadiliko ya kawaida kabisa,” alisema Mkwasa.
Mara ya mwisho, Cannavaro aliiongoza Stars akiwa nahodha baada ya kufungwa mabao 7-0 dhidi ya Algeria katika mechi ya kuwania kucheza Kombe la Dunia.

Serikali yaanza Msako wa 'Ma-Hausi Geli'
Klopp Aeleza Mikakati Ya Kusajili Mlinda Mlango Bora