Kocha Mkuu wa timu ya soka ya Taifa, Taifa Stars Charles Mkwasa amesema kuwa anashangaa kusikia kuwa, Nadir Haroub Cannavaro ameamua kujitoa timu ya taifa kwa sababu ya kuvuliwa unahodha wa timu hiyo.

Hivi karibuni Mkwasa alimpa unahodha mchezaji wa TP Mazembe ya Congo DR, Mbwana Samatta na kusema Haroub atabaki kuwa nahodha kwenye timu inayoshiriki michuano ya ndani ya Afrika (Chan).

Uamuzi huo ulimfanya Haroub kutangaza kujiuzulu kucheza timu ya taifa, akisema moja ya sababu ni kupokwa nafasi hiyo.

Akizungumza , Mkwasa amesema anamheshimu Haroub na anatambua mchango wake kwenye taifa.

“Sikuwa na sababu ya kumwondoa kwenye unahodha, mimi namheshimu sana Canavaro (Haroub) na ametoa mchango mkubwa kwa taifa hili na bado namhitaji, kwa nini nimuondoe,” alisema.

Samatta Arejea Lubumbashi Kumalizia Kiporo Chake
Chris Smalling Amkubali Kinda Borthwick-Jackson Hadharani

Comments

comments