Kocha mkuu wa timu ya Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa ametaja kikosi cha wachezaji 20 kwa ajili ya pambano la kukamilisha ratiba ya mechi za kuwania kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika.

Kuna mabadiliko machache katika kikosi hicho ukilinganisha na uteuzi uliopita kutokana na majeruhi na kushuka kwa viwango.

Mshambuliaji Thomas Ulimwengu pamoja na beki wa kulia, Juma Abdul wameachwa kutokana na majeruhi.

Kiungo Mwinyi Kazimoto ametemwa na nafasi yake kuchukuliwa na chipukizi Muzamiru Yassin wa Simba.

Simon Msuva pia amerudishwa katika kikosi huku David Kaseke akitemwa.

Kikosi Kamili:

Walinda Mlango: Deogratius Munishi na Aishi Manula.

Walinzi: Kelvin Yondani, David Mwantika, Vincent Andrew,  Shomari Kapombe, Mwinyi Haji na Mohamed Hussein.

Viungo: Jonas Mkude, Himid Mao, Muzamiru Yassin, Shiza Ramadhan, Farid Mussa, Simon Msuva.

Washambuliaji: John Bocco, Mbwana Samatta na Ibrahim Hajib.

 

Kamanda Sirro azungumzia undani wa tukio la Majambazi kuua Polisi wanne Dar
Mwanariadha Wa Ethiopia Asaidiwa