Aliyewahi kuwa Mchezaji na Kocha wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans, Charles Boniface Mkwasa amesema pamoja na kiwango kizuri walichoonyesha wachezaji wapya wa klabu hiyo lakini viongozi wanapaswa kuongeza Mshambuliaji kwa ajili ya kufunga mabao.

Mkwasa ambaye pia amewahi kuwa Katibu Mkuu wa Klabu hiyo amesema mbali na wachezaji wapya kuonyesha uwezo wao lakini bado Young Africans inahitaji Mshambuliaji ambaye atakuwa na uwezo wa kufunga kama alivyofanya Fiston Kalala Mayele msimu uliopita.

Amesema kwake amefurahishwa na kiwango cha juu kilichoonyeshwa na winga Maxi lakini anaamini bado anatakiwa kupewa msaada zaidi ili azalishe mabao mengi zaidi.

“Furaha ya mashabiki ni kuiona timu yao inapata mabao ndio watakuelewa, Musonda siyo mchezaji mbaya lakini bado atahitaji muda kuwa sawa, Young Africans wanaenda kwenye michuano ya kimataifa hivyo watahitaji kuongeza straika mwingine wa kusaidiana naye pale mbele kama ilivyokuwa kwa Mayele msimu uliopita,” amesema Mkwasa

Mkwasa ambaye amewahi kuwa pia kocha wa timu ya Taifa, Taifa Stars amewahi pia kuwa katibu mkuu wa timu hiyo. Yanga inahusishwa na mfungaji bora wa Cameroon, Dikongue Mahop na inasemekana atasaini punde.

CECAFA: Kagame Cup haitachezwa 2023
Hakim Ziyech aenguliwa Chelsea