Kocha mkuu wa Timu ya soka Taifa ya Tanzania (Taifa Stars)  Charles Boniface Mkwasa ametembelea  kwenye darasa wanalokutana makocha mbali mbali wa Soka visiwani Zanzibar  katika skuli ya Sekondari ya Haile Selasies na kuwapiga msasa wa siku moja pamoja na kubadilishana mawazo na makocha hao.

Mkwasa alifurahishwa mno baada ya kupata mualiko kutoka kwa Chama cha Makocha Zanzibar (ZAFCA) kwa kuwatembelea makocha hao ambapo huwa na kawaida ya kukutana mara kwa mara.

“Nimefurahi kupata mualiko kama huu kukutana na makocha wenzangu wa hapa visiwani , na pia nimependa utaratibu wenu wa kukutana mara kwa mara makocha nyote wa hapa visiwani kwa kubadilishana mawazo na kupeyana elimu ya ukocha, na mimi ntawashauri wenzangu kule bara tufanye kama hivi. Alisema Mkwasa.

Mbali na kuwapiga msasa makocha hao mtandao huu ukataka kujua kwa mwalimu huyo kuhusu kombe la Mapinduzi lililohitimishwa leo hii kati ya Mtibwa Sugar na URA ya Uganda huku akikiri  kuwa kweli vipaji vipo visiwani kwenye michuano hiyo pia akiipa tano timu ya JKU.

“ Vipaji vipo vingi sana hapa Zanzibar, kuna vijana nimewaona na ntawaita muda utakapofika, nimewaona kwenye timu zote tatu zilizoshiriki Mapinduzi kutoka Zanzibar, Jamhuri wapo nimewaona, Mafunzo pia nimewaona, na hata JKU wapo wengi wana vipaji”.Alisema Mkwasa.

Breaking News: Jerome Valcke Atimuliwa FIFA
Pellegrini: Vincent Kompany Sio Wa Leo Wala Kesho