Kocha msaidizi wa Young Africans, Charles Boniface Mkwasa amesema amegundua mambo mawili, baada ya kuanza mazoezi ya kikosi cha klabu hiyo jana jioni.
Kikosi cha Young Africans kilianza mazoezi ya kwanza jana jioni katika uwanja wa shule ya sheria, jirani na kituo cha daladala cha Ubungo Mawasiliano (Simu 2000), jijini Dar es salaam.
Mkwasa amesema jambo la kwanza ambao ameliona kwa wachezaji wake kuwa walikuwa wakifanya mazoezi ya nguvu zaidi, wakati shughuli za michezo zilipokua zimesimama kupisha vite dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona.
Amesema wachezaji wengi kati ya walioanza mazoezi hawa walikuwa wakifanya mazoezi ya nguvu kuliko kucheza mpira.
“Kwa maana hiyo ni shida ya kwanza ambayo imeonekana kwetu katika mazoezi ya leo (Jana) ambayo tutakwenda kulifanyia kazi,” alisema.
“Tatizo hilo limetokana na wachezaji kuonekana kufanya mazoezi ya nguvu kama ‘beach’ na maeneo mengine.”
“Jambo la pili ambalo nimeliona wachezaji wangu wengi wamepoteza uwezo wa kumiliki mpira kwani mchezaji akiwa na mpira mguuni inakuwa ngumu kuwa salama kwa asilimia kubwa na badala yake hupoteza.”
“Wakati huo huo nimeona wachezaji wakipoteza pasi mara kwa mara na limetokana kupoteza uwezo wa umiliki mpira.”
“Kama benchi la ufundi tumeliona hilo na tunazidi kulifanyia kazi ili kila kitu kwenda sawa,” alisema kocha huyo mzawa.

Leo asubihi kikosi cha Young Africans kimeendelea na mazoezi katika uwanja wa shule ya sheria, jijini Dar es salaam.