Aliyekuwa Mlinda Lango wa Simba SC, Mbrazil Jefferson Luis amepata dili jipya baada ya kusaini mkataba wa mwaka mmoja na timu ya Athletic Club ya nchini kwao.

Luis amesaini mkataba huo baada ya kupona majeraha ambayo aliyapata akiwa Simba SC hali iliyofanya avunjiwe mkataba.

Mlinda Lango huyo alisajiliwa na Simba SC ikiwa nchini Uturuki Julai mwaka huu kwa maandalizi ya msimu huu (pre-seasson) lakini hakumaliza hata juma moja ndani ya kikosi hicho, akaachwa na sasa amepata timu.

Simba SC ilimpa mkataba wa miaka miwili Jefferson lakini ililazimika kuvunja mkataba huo, baada ya Mlinda Lango huyo kuumia na kutarajiwa kupona baada ya miezi mitatu hadi minne.

Kiufupi Mbrazil huyo hakutua Bongo yalipo masikani ya Simba SC, aliishia Uturuki kambini tu kisha kurudi kwao Brazil kujiuguza.

Luis alisajiliwa na Simba SC ili kuziba pengo la Aishi Manula aliyekuwa majeruhi (sasa amepona), lakini baada baada ya kuachana naye, Simba SC ilisajili makipa wawili kwa mpigo ikianza na Hussein Abel kutoka KMC na Mmorocco, Ayub Lakred ambao hata hivyo hawajaonyesha makali langoni kwa Mnyama hadi Manula amerejea mzigoni.

Kalenda ya FIFA kuibadilisha Mtibwa Sugar
Majeraha yaharibu dili la Thomas Partey