Waziri wa Kazi, Ajira na Mahusiano ya Viwanda nchini Uganda, Kanali mstaafu Charles Okello Engola ameuawa kwa kupigwa risasi na mlinzi wake ambaye pia dakika chache baadaye alijiua kwa kujipiga risasi huku ikidaiwa kuwa alikuwa akilalamikia kutolipwa mshahara.

Kanali Engola ameuawa nyumbani kwake Kyanja jijini Kampala, na mlinzi wake huku baadhi ya walioshuhudia tukio hilo wakisema, mlinzi huyo alizunguka katika eneo hilo akifyatua risasi hewani mara baada ya kutekeleza mauaji hayo.

Naibu msemaji wa polisi wa Kampala Metropolitan, Luke Owoyesigire amethibitisha kutokea kwa tukio hilo huku Spika wa bunge la Uganda, Anita Among naye akithibitisha tukio hilo wakati akiendesha kikao cha bunge.

Aliyekuwa Waziri wa Kazi, Ajira na Mahusiano ya Viwanda nchini Uganda, Kanali mstaafu Charles Okello Engola enzi za uhai na mara baada ya kupigwa risasi. Picha ya Edhub.

“Asubuhi hii nimepokea taarifa za kusikitisha kuwa Mheshimiwa Engola ameuawa kwa kupigwa risasi na mlinzi wake, ambaye pia amejiua, Amesema Among,” alisema Spika Anita huku mmoja wa walioshuhudia tukio, akisema mlinzi huyo hakuwa amelipwa mshahara wake kwa muda mrefu.

“Alisema kuwa hakuwa amelipwa, alisema ana mke ambaye ni mjamzito na watoto wake hawakuwa wanaenda shuleni wakati wa muajiri wake watoto walikuwa wanaenda, alisema mmoja wa mashuhuda wa mauaji ya Waziri Engola aliyewahi kuhudumu pia kama Naibu waziri wa Ulinzi.

Man City yashtuka Ulaya, yamwita mezani Haaland
Mitego mizito ya Mtibwa Sugar Ligi Kuu