Maafisa wa usalama nchini Taliban, wamesema mlipuko wa bomu uliotokea katika shule ya kidini kaskazini mwa Afghanistan, umesababisha vifo vya wanafunzi wasiopungua 10.
Mlipuko huo, ulitokea wakati wa sala ya mchana katika Madrasa ya Al Jihadi mjini Aybak, ambao ndiyo mji mkuu wa mkoa wa Samangan ambapo wengi wa wanafunzi waliofariki ni wavulana.
Kwa mujibu wa picha za video zilizotolewa na Taliban kwa vyombo vya habari, zimeonesha eneo la mlipuko, ukumbi uliojaa vifusi, mikeka na viatu, kukiwa na maiti na damu iliyotapaa sakafuni.
Msemaji wa Wizara ya mambo ya ndani Abdul Nafi Takor, amesema wanafunzi kadhaa pia wamejeruhiwa katika shambulio hilo katika mkoa huo wa Samangan una wakaazi wengi zaidi wa kabila la Uzbek.