Nchi tano za Mashariki na Kusini mwa Afrika zinakabiliwa na mlipuko wa ugonjwa wa Kimeta huku zaidi ya watu 1,100 washukiwa kuambukizwa na vifo 20 vimetokea mwaka huu.

Shirika la Afya Duniani – WHO, limesema jumla ya visa 1,166 vya maambukizi vimeripotiwa katika nchi za Kenya, Malawi, Uganda, Zambia na Zimbabwe, huku visa 37 vikithibitishwa na vipimo vya maabara.

Zambia ilikuwa na hali mbaya zaidi tangu mwaka 2011 na Malawi iliripoti kisa chake cha kwanza kwa binadamu mwaka huu 2023, huku Uganda ikiwa na vifo 13.

Kimeta, kawaida huathiri mifugo kama Ng’ombe, Kondoo, Mbuzi pamoja na mimea ya msituni na Binadamu wanaweza kuambukizwa kwa kukaa karibu na Wanyama hao au bidhaa za wanyama zilizoharibika.

Wafanyabiashara wahimizwa mbinu mbadala za ulinzi
Majeraha yatajwa kuichawia Chelsea