Vyombo vya Habari nchini Afrika Kusini vimeripoti kutokea kwa Mlipuko katikati mwa jiji la Johannesburg ambao umeleta uharibifu mkubwa wa barabara, mali na kujeruhi watu 41, na kuzusha taharuki kwa jamii ya watu waishio eneo hilo na jirani
Huduma za dharura za awali zililaumiwa kutokana na kusua kwake, huku mabomba ya gesi chini ya ardhi yakitajwa kusababisha hali hiyo, lakini kampuni ya Egoli Gas ilisema ni jambo lisilowezekana kwani mlipuko huo ulipasua lami na kupindua magari kadhaa.
Hata hivyo, bado chanzo na hasara iliyopatikana haijatajwa rasmi huku Egoli Gas ikisema, “Mtandao wetu haujapata hasara ya shinikizo jambo linaloashiria mabomba ya gesi hayajakamilika. Wateja wetu katika eneo hilo wanaendelea kupokea gesi bila kukatizwa.”
Waziri Mkuu wa mkoa wa Gauteng unaojumuisha jiji la Johannesburg na Pretoria, Panyaza Lesufi alisema kitendo hicho ni muujiza kwani hakuna mtu alioyefariki na kwamba watu 41 waliojeruhiwa, wawili wapo katika hali mbaya, tisa kujeruhiwa vibaya na 30 na majeraha madogo.
Zifuatazio ni baadhi ya picha za matukio mbalimbali ya maeneo yaliyoathiriwa.