Watu 16 wamefariki dunia na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya kupasuka kwa bomba la chini ya ardhi la gesi karibu na msikiti mmoja mjini Dhaka, nchini Bangladesh.

Mkuu wa polisi katika eneo hilo, Zayedul Alam anasema tukio hilo limetokea usiku wa Ijumaa wakati waumini wa dini ya Kiislamu wakimaliza ibada yao katika msikiti wa Baitus Salat Jame.

Wakati hosipitali zikiendelea na matibabu ya takribani watu 37 ambao wanaelezwa kuungua kwa kiwango cha asilimia 90 ya miili yao, polisi ya Bangladesh ipo katika jitihada za kutafuta chanzo cha mlipuko huo.

Ni uzushi, hakuna dawa iliyoondolewa - NHIF
Agnes wa ITV kuzikwa kesho Tanga