Robert Chelsea ndiye Mmarekani mweusi wa kwanza duniani na mtu wa 40 kufanyiwa pandikizi la uso mzima julai mwaka huu, tangu mapandikizi ya aina hiyo kuanza mwaka 2015.
Upandikizaji huo uliofanyiaka kwa saa 16 chini ya uangalizi wa timu ya madaktari 45 ndio ulioonekana kuwa na mafanikio makubwa zaidi duniani.
Kabla ya hapo alifanyiwa upasuaji kwa zaidi ya mara 30 bila mafanikio, lakini upasuaji wa 31 ambao alifanyiwa hospitali ya Boston’s and Women’s. umeweza kuwa wa matumaini na mafanikio makubwa kwani hadi sasa anaendelea vizuri.
Chelsea alipata ajali mwaka 2013 baada ya gari lake kugongana na gari jingine ambalo dereva wake alikuwa amelewa pombe na kusababisha apoteze uso wake pamoja na sehemu nyingine nyingi za mwili wake.