Mwanzilishi na mmiliki wa Facebook, Mark Zuckerberg amesema kuwa haoni sababu ya mtandao huo kuanza kuchuja taarifa zinazotolewa na wanasiasa au taarifa zinahusu masuala ya demokrasia.

Akizungumza jana jijini Washington DC baada ya wiki kadhaa za kukosolewa sana kufuatia uamuzi wa kampuni yake kutoyafungia matangazo ya kisiasa ambayo wengi wameeleza kuwa hubeba taarifa zisizo za kweli.

Alisema kuwa kampuni yake itaendelea kuwa ngazi ya kisiasa ikitoa nafasi kwa wanasiasa wote, lakini anaamini uamuzi huo lazima utawafaidisha wanasiasa wote ambao mtandao huo bila kujali usahihi wa taarifa zao.

“Tuko kwenye barabara nyingine za kuvuka. Tunaweza kusimama kwa ajili ya haki ya kujieleza bura, kwa kuelewa matatizo yanayoweza kuja na haki hiyo lakini tunafahamu kuwa safari ndefu kuelekea mafanikio inahitaji mawazo ambayo yanatupatia changamoto,”alisema Zuckerberg.

“Na hata kama mnapenda au hampeni. Ninadhani tunahitaji kutambua kilichopo na kusimama pamoja kutoa sauti na kujieleza bure katika kipindi hiki kigumu,”aliongeza.

Alikumbushia kuhusu tukio la Martin Luther King Jr, kufungwa jela Birmingham, Alabama kama mfano wa matokeo yasiyo mazuri ya uhuru wa kujieleza.

Lakini mfano huo ulimuibua binti wa Martin Luther King Jr, aliyeeleza kuwa taarifa za uongo zilizosambazwa na wanasiasa ndizo zilisababisha baba yake kuuawa.

Lori la mafuta laanguka na kulipuka, laua na kuteketeza nyumba, soko Nigeria
Video: Harmonize kupanda jukwaani fiesta 2019, amemaliza bifu lake na Clouds