Tajiri mmoja na Mmiliki wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya ‘John The Baptist’ iliyoko Boko Jijini Dar es salaam amejiua kwa kujipiga risasi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Jumanne Murilo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, ambapo amesema kuwa Ndibalema Mayanja alijifyatulia risasi kwa bahati mbaya wakati akisafisha silaha yake.
Amesema kuwa Ndibalema Mayanja alikuwa ni Kapteni Mstaafu wa Jeshi la Wananchi Tanzania, (JWTZ) na alijiua kwa bastola aina ya Short-gun aliyokuwa akiimiliki.
“Mayanja alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa saratani kwa muda wa miaka 15 kwa mujibu wa familia yake na alikuwa anatamka kwamba anataka kujiua, na aliomba silaha hiyo kwa ajili ya kuisafisha lakini baadae alijielekezea kifuani na kujifyatulia risasi,”amesema Kamanda Murilo
Hata hivyo, msemaji wa familia, Steven Gumbo amesema kuwa Mayanja alijipiga risasi kwa bahati mbaya wakati akisafisha silaha zake.