Mmiliki wa shule ya malezi ya watoto ‘’daycare’’ January Neatherlin (32) ametupwa jela kwa miaka 21 kwa tuhuma za kuwapa watoto vidonge vya usingizi aina ya ‘’melatonin’’ ili aendelee kufanya mazoezi ya viungo bila kusumbuliwa na watoto hao.
January amehukuwa kifungo hiko kwa kosa la kulea watoto kwa njia isiyo halali kwa kuwanywesha watoto wadogo dawa ya usingizi.
Mkuu uyo amekuwa akifanya hivyo kwa muda wa miaka 4 huku akiwadanganya wazazi wa watoto hao kuwa amepitia mafunzo ya unesi.
Polisi walipata taarifa hiyo kutoka kwa mtu wa karibu wa shule hiyo, ndipo walipochukua uamuzi wa kwenda kufanya uchunguzi kubaini uhalifu huo unaofanywa dhidi ya watoto wadogo.
Ambapo polisi wamesema kwamba wamemuona mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 32, akiondoka nyumbani hapo mara mbili baada ya kuwa mwangalizi wa watoto hao.
Katika safari hizo mbili ambazo alikuwa anatoka watoto aliowaacha shuleni hapo na kuwapa vidonge vya melatonin ili walale usingizi na yeye aendelee na safari zake.
Mmiliki huyo aliwaarifu wazazi wa watoto hao wasije kuwachukua watoto wao kuanzia saa 5 hadi saa 8 akidai kuwa muda huo watoto hutumia kupumzika.
Ndipo polisi walipomtembelea na kumkuta muda huo anautumia kwenda kufanya mazoezi ya viungo baada ya kuwanywesha watoto vidonge hivyo vya usingizi.
Hivyo mwanamama huyo anashikiliwa na polisi na mahakama nchini humo imemfungulia mashtaka atakayotumikia jela kwa muda wa miaka 21.