Klabu ya Geita Gold imeinasa saini ya kwanza kwenye dirisha hili baada ya kumsajili, Tariq Simba kwa mkataba wa miaka miwili.

Kiungo huyo amejiunga na kikosi hicho baada ya mkataba wake na Polisi Tanzania iliyoshuka daraja kumalizika.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Geita, Simon Shija alisema hawezi kuweka wazi sajili ambazo hadi sasa wamezinasa hadi pale watakapokamilisha utaratibu mzima ndipo watatangaza.

“Ni kweli tumefanya maboresho ya kikosi chetu kama ilivyokuwa utaratibu kwenye kila msimu ambapo dirisha linakuwa wazi, bado hatujakamilisha wote tunaowahitaji ila baadhi tumewasajili,” amesema.

Hata hivyo, licha ya Shija kutotaka kuweka wazi ila Mwanaspoti linatambua nyota huyo mwenye uwezo mkubwa wa kucheza kiungo wa chini na juu ataichezea timu hiyo kwa msimu ujao. Usajili huo ni wa kwanza kwa kikosi hicho baada ya kuondokewa na mastaa wengi.

Gwiji Mtibwa Sugar kutua Ihefu FC
Kocha Simba SC azionya Klabu Ligi Kuu 2023/24