Mbunge wa Mbogwe CCM, Nicodemas Maganga amehoji iwapo ni kweli mawaziri wanamsaidia Rais Samia Suluhu Hassan katika utendaji wao wa kazi na si kumsifia Rais kwamba anaupiga mwingi.
Maganga ameyasema hayo Bungeni jijini Dodoma na kueleza kwamba kama mawaziri wangekuwa wanamsaidia kikamilifu Rais Samia kikamilifu, ripoti za Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), zisingekuwa na ukakasi.
Amesema, kitendo cha Rais Samia kuonesha kukasirishwa na ubadhirifu ulioibuliwa na ripoti ya CAG, ni kiashiria kimojawapo kuwa wasaidizi wake hawamsaidii kikamilifu na hivyo kupelekea madudu mengi kujitokeza wakati wa ukaguzi.