Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa ametangazwa mshindi wa uchaguzi mkuu wa urais nchini Zimbabwe kwa mujibu wa tume ya uchaguzi ya nchi hiyo.
Katika majimbo 10 yote yalioyotangazwa, Mnangagwa ameshinda kwa asilimia 50.8, dhidi ya asilimia 44.3 alizopata mgombea wa chama cha upinzani Nelson Chamise.
Aidha, Mwenyekiti wa Chama Cha MDC Alliance, Nelson Chamisa amesema kuwa kuhesabiwa kwa kura hakukufanyiwa uhakiki.
Chamisa amesema kuwa ZANU-PF haikushinda uchaguzi huo, bali wanajaribu tuu kupitisha suala lisilo na ukweli, na ameahidi kupambana na suala hilo.
Hata hivyo, Kwa upande wa Muungano wa Afrika, umesema kuwa uchagauzi huo ulikuwa huru na wa haki na haukuwa na tatizo lolote.