Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Jokate Mwegelo amekemea hatua ya Wafanyabiashara wanaoficha mafuta Wilayani humo, wakilenga kusubiria mabadiliko ya bei kwa lengo la kuuza cha juu na kuwataka kuacha mara moja kwani kitendo hicho ni kuhujumu uchumi na pia kinaichafua Serikali.

Jokate ameyasema hayo hii leo July 31, 2023 baada ya kutembelea Kituo cha Mafuta Mombo High Way, ambacho hakijafanya kazi kwa siku ya tatu wakidai kuwa Pampu imeharibika.

Amesema, “kuna maeneo tunajua kuna changamoto lakini hapa mafuta mnayo leo siku ya tatu Wananchi hawapati huduma, hii haikubaliki, kuna Watu wanaficha mafuta wakisubiria mabadiliko ya bei, sasa kama Serikali hatuwezi kuruhusu Wananchi waumie.”

Aidha, Jokate ameongeza kuwa, “nimeongea na fundi wa pump, aje atengeneze na nitakuja tena usiku nikifika nataka nikute pump inafanya kazi Wananchi wanahudumiwa sitaki kukuta sababu, hatuwezi kukubali Serikali ichafuliwe kirahisi, kinachofanyika hapa ni kuichafua Serikali.”

Watanzania wapo tayari uwekezaji, mabadiliko Bandari - Chongolo
Mkutano Bukombe: CHADEMA imekata pumzi?