Mbunge wa Jimbo la Geita, Joseph Musukuma amesema wanaisubiri ripoti ya CAG Bungeni ili wahusika wa ubadhilifu waliotajwa kwenye ripoti hiyo ambao wameisababishia hasara Serikali waweze kuwajibishwa.

Msukuma ameyabainisha hayo wakati akichangia azimio la Bunge la kumpongeza Rais Dkt. Samia kwa kuimarisha Demokrasi nchini na kukuza Diplomasia ya uchumi na kusema haipendezi Wabadhilifu kutajwa na CAG kila mwaka bila ya kuchukuliwa hatua zozote.

Amesema, “mnatutengenezea uadui, bora myamalize wenyewe, tunataja watu hawachukuliwi hatua ntu anachukua kesi anaenda kuipaki TAKUKURU haiwezekani tumejadili haya mwaka jana tukataja Watu yaani kesi ya mwaka jana inakutwa na ya mwaka huu. tumsaidieni Rais.”

Aidha, Msukuma ameongeza kuwa Rais amefika hatua ya kusema neno pumbavu na kuhoji iwapo wanataka asome taarifa ya mwakani akiwa na kiboko mkononi endapo Bunge halitachukua hatua za kumsaidia ili kuondokana na kesi za aina hiyo.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo April 5, 2023
Ongeza kipato kusanya mgao wa Tsh 5m kutoka Meridianbet