Mwili wa Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Godfrey Mngereza, umewasili jijini Dar es salaam leo Jumatatu Desemba 28, 2020.

Shughuli za Ibada na kutoa heshima za mwisho zimeendeshwa leo nyumbani kwa Marehehmu Kibamba Luguruni Dar Es Salaam.

Taarifa iliyotolewa na BASATA imeeleza kuwa, mwili wa Mngereza utaagwa kesho Jumanne katika ukumbi wa Karimjee na mazishi yatafanyika Desemba 30, 2020 kijijini kwao Suji wilayani Same mkoani Kilimanjaro.

Mngereza amefariki dunia Desemba 24 mwaka huu katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Dodoma alikokuwa akipatiwa matibabu katika chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi wa karibu (ICU).

Hillary, Kabunda warudi KMC FC
Sven: Naomba vyombo vya habari, mashabiki na wanachama kuacha kukosoa