Kiasi cha Shilingi Bilioni 2, kilichotengwa na Serikali kwa ajili ya mikopo kimeanza kufanya kazi baada ya Mfanyabiashara Shaban Ally kupatiwa mkopo wa Shiling Milioni 50 na Waziri wa Nishati, January Makamba zitakazomsaidia kukuza biashara yake ya Mafuta.
Waziri Makamba, ambaye bado yuko kwenye ziara ya Kijiji kwa Kijiji ametoa kiasi hicho cha pesa mara baada ya kuzungumza na Wananchi, wakati akiwa katika Kijiji cha Ugaka kilichopo Wilayani Igunga Mkoani Tabora.
Shaban Ally, ni Kijana ambaye anafanya biashara ya mafuta ya kupima kwenye chupa na madumu kwenye Kijiji hicho na kabla ya kupatuwa mkopo huo pia alipata wasaa wa kuzungumza na Waziri huyo wa Nishati.
Waziri Makamba amesema, “Basi sisi tutakukopesha Milioni 50, maana tumetenga Bilion 2 kama sehemu ya majaribio kwa mwaka huu wa fedha sababu ni kwamba Wananchi Vijijini wanateseka kupata mafuta ambayo si salama na kwa bei ya juu.”
- Waliovujisha siri ununuzi wa gari la Spika kwa bilioni 3 kukiona
- Shaban Ally anakuwa mnufaika wa kwanza atakayepata fedha za mkopo zilizotengwa na Serikali kupitia wakala wa Umeme REA, ili kuwawezesha wajasiriliamali kufungua vituo vidogo vya mafuta vijijini, kuuza mafuta safi, kwa njia salama na kwa bei elekezi.