Shirikisho la Soka nchini Tanzania ‘TFF’ limewataka Wanasheria wake kuchukua hatua dhidi ya Mmiliki wa Klabu ya Gwambia FC na Kituo cha Radio cha Clouds FM, kwa madai ya kutoa shutuma za uongoo dhidi ya Shirikisho hilo.
Mmiliki wa Gwambina FC Alexander Mnyeti anadaiwa amelishutumu Shirikisho hilo kupitia Clouds FM baada ya kufanyiwa mahojiano, kuhusu taarifa za klabu yake kujiondoa katika ramani ya Soka nchini Tanzania.
Katika mahojiano hayo Mnyeti alisema:”Ligi ilikuwa ngumu kwa sababu ilipaswa tushuke na ikiwezekana tupotee kabisa Duniani,”
“Viongozi wa Bodi ya Ligi walikuwa wanahitaji sana hela ata tulivyokuwa ligi kuu nasikitika kuongea haya lakini hakuna namna, huku chini kuna uozo kuna watu pale Bodi ya ligi wameukamata huu mpira kama mali yao, 2021 ligi ilikuwa ngumu kwa sababu ilikuwa ni maelekezo lazima Gwambina ashushwe daraja,”
“Watu wanataka pesa kwa nguvu, tusipotowa pesa lazima tushuke zaidi, sisi hatukuweza kutoa pesa sababu hatukuwa na pesa, haiwezekani mimi niwalishe wachezaji, niwatibu niwasafirishe na wewe kiongozi nikulipe, kumbe chuki ilianza kwenye michezo ya Simba SC na Young Africans walikuwa wanalazimisha michezo hiyo tukacheze CCM Kirumba, wakati sisi tuna uwanja wetu, ulikuwa ni mpango wa kuiba mapato”
Katika taarifa yake TFF imeeleza kuwa: “Gwambia kabla ya kutangaza kujitoa ilikua inacheza Ligi Daraja la Kwanza (Championship), na Uwanja wake wa nyumbani ulioko Misungwi mkoani Mwanza ulizuiwa kutumika kwa michezo ya Ligi hiyo kwa kutokidhi vigezo.”
“Tunavikumbusha vyombo vya habari kuzingatia misingi ya taaluma hiyo ikiwemo kutotoa habari zenye shutuma bila kusikiliza upande wa pili.”