Mbunge wa Kibamba kwa tiketi ya Chadema, John Mnyika amesema kuwa bomoabomoa iliyofanyika Kimara jijini Dar es salaam, ni haramu kwasababu sheria iliyotumika ilitungwa mwaka 1932 na ilishafutwa.

Amesema kuwa Rais Dkt. Magufuli katika ziara yake ya Mwanza alitoa kauli ya kibaguzi na kama si ya kibaguzi basi serikali itoe kauli ya kuwalipa fidia wakazi hao waliobomolewa nyumba zao.

“Kwasababu Serikali ilisingizia sheria lakini mimi kama mbunge nilichukua hatua ya kuleta marekebisho ya sheria bungeni ili barabara yote iwe mita 60, lakini serikali ikafanya njama na katibu wa bunge (Thomas Kashilillah) kuzuia huo mswaada,”amesema Mnyika

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi, Elias Kuandikwa amesema kuwa sheria mbalimbali za barabara zilipokuwa zikitungwa zilikuwa zinazingatia maendeleo hivyo sheria ya mwaka 1932 iliainisha ukubwa wa barabara popote ilipokuwa inajengwa.

Hata hivyo, Kwandikwa amemtaka mbunge huyo kuwasiliana na mamlaka ya halmashauri za serikali za mitaa ambao ndio wasimamizi kuona kama kuna mahitaji kwa baadhi ya maeneo kufanyiwa marekebisho ya sheria hiyo.

Usajili timu za wanawake watangazwa
Serikali kupiga mnada ng'ombe 10,000