Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Klabu ya Simba SC na Mwekezaji Mohammed Dewji ‘Mo’ amesema ili kuhakikisha wanafikia malengo yao waliyoyaweka msimu huu katika michuano hiyo ya kimataifa wanahitaji kujipanga kimbinu na kuzidisha mapambano ili kufanya vema katika mchezo wao wa hatua ya pili ya Ligi Mabingwa dhidi ya FC Platinum ya Zimbabwe.

Jumamosi Desemba 05, Simba SC ilisonga mbele kwenye michuano hiyo mikubwa Barani Afrika, kufuatia kulazimisha suluhu ya bila kufungana katika mchezo wa marudiano wa Ligi Mabingwa Afrika dhidi ya Plateau United kutoka nchini Nigeria.

‘Mo’ amesema japokuwa yeye si kocha lakini wanahitaji kufanya mazoezi zaidi ili kuwa bora, kabla ya kuwakabili FC Platnum ambao wataanzia nyumbani mjini Bulawayo, Zimbabwe kati ya Desemba 22 au 23 katika uwanja wa National Sport na kisha watarudiana kati ya Januari 5 au sita katika uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es salaam.

Amesema, katika mchezo wa Jumamosi kikosi cha Simba SC kilikosa magoli mengi, huku kkishindwa kutumia nafasi za mipira ya adhabu ndogo, ikiwemo kona zaidi ya 10 lakini wachezaji wao hawakuweza kutumia nafasi hizo kupata goli.

Amesema, jambo kubwa kwa sasa ni timu yao kufanikiwa kuvuka kwenye raundi ya kwanza hivyo wanarudi kwenye mikakati na akiwa kama Mwenyekiti atapambana kuhakikisha anapambana na hivyo hivyo kwa wachezaji huku pia akiwataka mashanbiki kuendelea kuiunga mkono timu yao.

Simba imetinga hatua hiyo kwa jumla ya goli 1-0 walilopata katika mchezo wa awali uliochezwa Novemba 29 katika uwanja wa New Jos huku Platinum wakiwafunga Costa do Sol ya Msumbiji jumla ya mabao 4-1 baada ya kushinda 2-1 na kisha kushinda goli 2-0 katika mchezo wa marudianoa uliochezwa leo kwenye mji wa Bulawayo.

Wakamatwa wakitapeli watu kwa jina la 'Usalama wa Taifa'
Ni mvurugano ACT Wazalendo