Siku chache baada ya Jarida la Forbes kumtaja Mwenyekiti mtendaji wa makampuni ya METL, Mohammed Dewj kuwa tajiri namba 21 Afrika na namba moja Tanzania, limemtunuku tuzo.

Jana Jarida hilo lilimkabidhi Mo Dewj tuzo ya ‘Africa’ s Personal of The Year 2015′ akimshinda Rais wa Nigeria, Muhammudu Buhari na wengine watatu waliokuwa wakiiwania tuzo hiyo.

Baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo, Dewj alisema kuwa anaielekeza tuzo hiyo kwa vijana wa Tanzania.

Kwa mujibu wa Forbes, Dewj ni Mtanzania pekee bilionea mwenye utajiri wa dola bilioni 1.1.

TRA wawacharukia wafanyabiashara, wapiga Makufuli Maduka
Video: Boss Wa Empire Alazimika Kuelezea Kitendo Cha Jamal (Shoga) 'Kum-Kiss' Msichana