Bilionea Mohammed Dewji maarufu kama Mo Dewji ametangaza kujiuzulu nafasi ya Uenyekiti wa Bodi ya Klabu ya Simba.

Ametangaza uamuzi huo leo usiku kupitia mtandao wa Twitter ikiwa ni dakika chache baada ya klabu hiyo kushindwa kutwaa Kombe la Mapinduzi ikipigwa 1-0 na Mtibwa Sugar kwenye mchezo wa Fainali ulioshuhudiwa visiwani Zanzibar.

Kwa mujibu wa maelezo yake, Mo ameonesha kutoridhishwa na matokeo hayo akiyalinganisha na kiwango kikubwa cha fedha zilizokuwa zimewekezwa kwenye mishahara ya kikosi hicho. Amesema kwa mwaka mmoja bajeti ya mishahara ilikuwa karibu Sh 4 Bilioni.

“Inasikitisha Simba hawakuweza kushinda. Baada ya kulipa mishahara inayokaribia Sh 4 bilioni kwa mwaka. Ninajiuzulu nafasi ya Uenyekiti wa Bodi na nitabakia kuwa muwekezaji. Simba nguvu moja. Nitajikita katika kuboresha miundombinu na shule ya mafunzo ya vijana,” tafsiri isiyo rasmi ya Tweet ya Mo Dewji aliyoiandika kwa lugha ya Kiingereza.


 

Video: Sakata la Meya Dar Sarakasi tupu, Joto sasa lazidi kuzua kihoro
Serikali kuanzisha kanzi Data ya taifa ya vinasaba (DNA) vya binadamu

Comments

comments